Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (MVP), Enock Morrison kutoka Ghana, ameripotiwa kuzikataa ofa kutoka kwa vigogo wa soka Tanzania, Yanga SC na Simba SC.
Taarifa zinaeleza kuwa Morrison amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu moja nchini Sudan, hatua iliyomaliza matumaini ya klabu hizo mbili kumsajili katika dirisha hili la usajili.
Mbali na Yanga na Simba, Singida Black Stars nayo ilikuwa miongoni mwa klabu zilizokuwa zikifuatilia kwa karibu huduma za kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa.
Uamuzi wa Morrison kuhamia Sudan unatajwa kuchangiwa na makubaliano mazuri aliyoyapata kutoka klabu hiyo, huku klabu za Tanzania zikilazimika kuendelea kutafuta mbadala katika soko la usajili.