Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amesema maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar yamekamilika na kila kitu kiko tayari kwa ajili ya pambano hilo muhimu.
Akizungumza kabla ya mchezo huo, Barker amesema Simba inautambua ubora wa Mtibwa Sugar na sababu zinazowafanya wapambane kwa nguvu katika kila mchezo.
“Maandalizi kwa upande wetu yapo vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo huu muhimu kwetu. Tunafahamu tunakwenda kucheza na timu inayopambana kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.”Kocha huyo ameongeza kuwa licha ya kuwaheshimu wapinzani wao, Simba itaingia uwanjani ikiwa na lengo moja tu la kuhakikisha inapata ushindi na alama tatu muhimu katika mbio za mafanikio msimu huu.