Ruka hadi maudhui
SOKALEO

JANGWANI YAPANIA KUMRUDISHA AZIZ KI, YATUMA OFA NONO

Chikao
JANGWANI YAPANIA KUMRUDISHA AZIZ KI, YATUMA OFA NONO
Taarifa kutoka Libya zinaeleza kuwa klabu ya Al-Ittihad imepokea ofa rasmi ya dola za Marekani 350,000 kutoka Yanga SC kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kuelekea msimu ujao.Inaelezwa kuwa Yanga na Aziz Ki tayari wamefikia makubaliano kuhusu mkataba pamoja na maslahi binafsi, jambo linaloifanya hatua iliyobaki kuwa makubaliano kati ya klabu hizo mbili.
Aidha, Aziz Ki mwenyewe anaripotiwa kuwasilisha ombi la kuondoka Al-Ittihad baada ya madai ya kutolipwa baadhi ya fedha zake zinazohusiana na usajili wake alipotua katika klabu hiyo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.Sasa macho ya mashabiki wa Yanga yanaelekezwa Libya kusubiri hatma ya mazungumzo hayo ambayo yanaweza kumrejesha nyota huyo Jangwani kwa mara nyingine.
Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Kocha wa Simba Steve Barker Awasha Moto Mpya

YAMAL: Afikisha mchango wa mabao 20 ndani ya mechi 13