Ubora wa simba katika kipindi hiki umekuwa maumivu makubwa kwa yanga. Tangu dirisha dogo la usajili, Simba wamefanya maboresho makubwa ndani ya kikosi chao kwa kusajili wachezaji walioingia haraka kwenye mfumo wa timu na kuendana vizuri na ushindani wa ligi.Tofauti kubwa ya Simba ya sasa na ile ya msimu uliopita ni uimara wa kikosi pamoja na ushindani mkubwa wa nafasi ndani ya timu.
Hilo limeifanya Simba kuwa na nguvu kubwa zaidi wanapokutana na Yanga.Ndiyo maana katika mechi za hivi karibuni Yanga wamekuwa wakipata wakati mgumu dhidi ya Simba, kwani “Mnyama”anaonekana kuwa na kiwango cha juu zaidi kwa sasa, kuanzia benchi la ufundi hadi ubora wa wachezaji waliopo uwanjani.