Ruka hadi maudhui
SOKALEO

MOLAN NA BOBEDI WAANZA KAZI RASMI YANGA

Chikao
MOLAN NA BOBEDI WAANZA KAZI RASMI YANGA

Klabu ya Young Africans SC imeanza rasmi maisha mapya chini ya makocha wa muda, Molan na Mabedi, ambao leo wameanza majukumu ya kuinoa timu hiyo kufuatia kuondolewa kwa aliyekuwa kocha mkuu, Pedro Gonçalves.

Makocha hao wawili wanatarajiwa kuiongoza Yanga hadi mwisho wa msimu huku wakipewa jukumu la kuhakikisha timu inaendelea kufanya vizuri katika mechi zilizobaki za ligi na mashindano mengine.

Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya uamuzi wa klabu kuachana na Pedro Gonçalves, jambo ambalo limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka nchini kutokana na umuhimu wa kipindi hiki cha mwisho wa msimu.

Mashabiki wa Yanga sasa wana matumaini kuwa ujio wa Molan na Mobedi unaweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya kikosi hicho na kusaidia timu kuendelea kubaki kwenye ushindani mkubwa.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Kocha wa Simba Steve Barker Awasha Moto Mpya

YAMAL: Afikisha mchango wa mabao 20 ndani ya mechi 13