Klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga) imetangaza rasmi kumfuta kazi Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Pedro Gonçalves, kufuatia maamuzi ya uongozi wa klabu hiyo.
Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Mei 6, 2026, uongozi wa Yanga umemshukuru kocha huyo kwa mchango wake ndani ya klabu na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo.
Katika kipindi hiki cha mpito, timu hiyo itaongozwa na makocha Abdihamid Moalin pamoja na Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu.
Hatua hiyo inaashiria mabadiliko ya kiufundi ndani ya kikosi hicho huku mashabiki wakisubiri kuona mustakabali wa timu yao katika mechi zilizosalia za msimu.