Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » SOWAH APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU SIMBA SC
    KITAIFA

    SOWAH APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU SIMBA SC

    ChikaoBy ChikaoMarch 3, 202601 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    UONGOZI wa klabu ya Simba SC umeweka wazi kuwa mshambuliaji wao, Jonathan Sowah, atapelekwa katika kamati ya nidhamu kwa ajili ya mahojiano na kupatiwa adhabu mara moja kutokana na matukio ya hivi karibuni.

    Hivi karibuni kulizuka sintofahamu pale mshambuliaji huyo alipoondolewa kambini kabla ya mchezo wa Kariakoo Derby, huku ikidaiwa kuwa hatua hiyo ilitolewa kutokana na utovu wa nidhamu.

    Tukio hili limeibua maswali miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo  huku uongozi ukihakikisha kuwa hakuwa na chaguo bali kufuata taratibu.

    Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, Kamati ya Nidhamu itakutana na Sowah pamoja na benchi la ufundi kwa ajili ya mahojiano ya kina.

    “Baada ya kikao hicho na kumsikiliza mchezaji tutatoa maamuzi ikiwemo kupewa adhabu au kukatwa kiasi cha fedha katika mshahara wake,” amesema Magori.

    Sowah ameondolewa kikosini mara baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi, ambapo alikosa mechi tano kutokana na amri hiyo.

    Hatua ya kupelekwa kwake kamati ya nidhamu inafuatia kanuni za ndani za klabu na kuonyesha wazi kuwa nidhamu ndani ya kikosi ni jambo lisilo na marudio.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleUWANJA WA MKAPA KUFUNGWA KUPISHA AFCON 2027
    Next Article BEI MBAYA AKIRI SIMBA IMEMFUNDISHA SOMO ZITO

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.