Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » YANGA WAINGIA UWANJA WA MKAPA WAKIWA NA MIKAKATI YA KUIFUNGA AZAM FC
    KITAIFA

    YANGA WAINGIA UWANJA WA MKAPA WAKIWA NA MIKAKATI YA KUIFUNGA AZAM FC

    ChikaoBy ChikaoMarch 15, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KUELEKEA mchezo wa kesho wa Der es Salaam Derby wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, Amesema  kuwa timu yake inakutana na changamoto kubwa dhidi ya wachezaji wenye viwango vya juu.

    Amesema kuwa watakutana na timu ngumu zaidi kwenye ligi hii, ambayo imejipanga vyema kwa mechi hiyo muhimu.

    “Timu yao ni imara sana, hasa ukizingatia ufanisi wao kwenye mashindano ya kimataifa. Tulicheza nao kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi, na nadhani wanapokuja kesho watakuwa wamejipanga vyema zaidi,” amesema Pedro.

    Kesho, Yanga wanakabiliana na Azam FC katika mchezo wa nyumbani, utakaochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambapo wanatafuta pointi tatu muhimu.

    Kocha Goncalves ameeleza kuwa kucheza kwenye uwanja wa Mkapa ni changamoto mpya kwa timu yake, kwani ni mara ya kwanza tangu awe kocha wa Yanga.

    “Kucheza uwanja wa Mkapa ni fursa nzuri sana kwetu. Uwanja huu ni mzuri, na tumejiandaa vyema ili kupata matokeo mazuri. Hakika kuna changamoto ndogo ndogo, hasa baada ya mchezo uliopita na safari nzima.

    Wachezaji watakabiliana na uchovu, lakini tumepata muda wa kufanya maandalizi ya kuweka miili sawa tayari kwa mapambano,” amesema Pedro.

    Kocha huyo pia amesisitiza umuhimu wa wachezaji kuwa na uelewa wa kimbinu, hasa wanapocheza katika viwanja tofauti.

    “Changamoto kubwa ni kucheza katika mazingira tofauti, unaweza kucheza kwenye uwanja mbaya au mzuri. Ni lazima wachezaji wawe na ufahamu mkubwa wa kimbinu ili kukabiliana na vikwazo vya viwanja,” ameongeza.

    “Wachezaji wangu wanafanya vizuri sana. Tokea nimeingia Tanzania, nimepata sare moja tu. Kwa kifupi, nina timu nzuri inayoweza kukabiliana na timu yoyote bila wasiwasi.

    “Ninaposema Azam ni bora, haimaanishi kuwa tunaenda kwa hofu. Tunajiamini, tuna timu bora, sisi ni Yanga. Tunawaheshimu, lakini tutacheza kwa kujituma na kwa nidhamu kubwa,”amesema  kocha huyo.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleTanzania Yatoa Zaidi ya Sh80 Bilioni CAF Ili Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027
    Next Article BAJABER ARUDI KWENYE RAMANI KUPITIA WITO WA TAIFA

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.