Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » MSHAMBULIAJI MTANZANIA ASIMULIA ATHARI IRAN
    KITAIFA

    MSHAMBULIAJI MTANZANIA ASIMULIA ATHARI IRAN

    ChikaoBy ChikaoMarch 3, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    WAKATI hali ya taharuki ikiendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Kati kufuatia mshambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran, imeripotiwa wachezaji watatu wa Kitanzania wanaokipiga katika ukanda huo wako salama.

    Wachezaji hao ni mshambuliaji Simon Msuva anayekipiga Al Talaba ya Ligi Kuu Iraq, Clara Luvanga (Al Nassr, Saudia) na Morice Sichone (Gulf FC, UAE).

    Taarifa ilizozipata Soka la Bongo ni kwamba, eneo alilopo Msuva ni salama na wanaendelea kama kawaida kucheza mechi mbalimbali kwani hadi sasa hakuna ripoti ya kushambuliwa.

    Ndugu wa Msuva, James Msuva anayekipiga Coastal Union ya Tanga, amesemawamekuwa wakizungumza mara kwa mara na nyota huyo na amewakikishia kazini kwake kuna usalama.

    “Ni kweli amesemakule hali iko shwari, wanasikia milipuko kwa mbali, lakini wapo salama kabisa, maisha yanaendelea na ligi haijasimama,” amesemana kuongeza.

    “Klabu imewahakikishia usalama, wanachokifanya sasa ni kuzingatia mpira na kufuata maelekezo ya mamlaka, ila tunachoshukuru kaniambia hali ni shwari kabisa.”

    Wakati Msuva hali ikiwa shwari, kwa upande wa mshambuliaji mwingine wa Kitanzania, Morice Sichone huko bado hakujakaa sawa kwani wameendelea kukaa ndani kwa ajili ya usalama zaidi.

    Akizungumza na Mwanaspoti, Sichone alisema: “Hata huku Dubai hali si shwari kabisa, hali mbaya sana tangu juzi saa tano kuna mabomu tu, yaani tunayasikia nje huko, jana kidogo yalipigwa matatu hali ilipopungua tukaenda kucheza mechi ya ligi.

    “Ingawa bado tupo ndani tu na tumezuiliwa kutoka nje bila sababu ya msingi kwa ajili ya usalama zaidi lakini wenyeji wanaendelea na shughuli zao.”

    Saudi Arabia anapocheza Clara, mapema jana mashambulizi yaliripotiwa, moto mkubwa katika kiwanda cha kusafisha mafuta ulionekana kabla ya kudhibitiwa kwenye eneo la Riyadh iliyopo kambi ya timu hiyo na Ras Tanura kwenye kituo kikubwa cha mafuta.

    Mmoja wa mchezaji huyo, Amosi Mlandali aliliambia gazeti hili kuwa: “Clara aliondoka jana kujiunga na timu ya taifa iliyoweka maskani yake Dubai wanapojiandaa na mashindano ya WAFCON, nahisi kama yalitokea basi alikuwa tayari ameondoka.”

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleKUELEKEA DABI YA KARIAKOO……YANGA MAPEMAAAA TU…..SHILINGI IKO JANGWANI KITAMBO
    Next Article UWANJA WA MKAPA KUFUNGWA KUPISHA AFCON 2027

    Related Posts

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    April 26, 2026

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    April 25, 2026

    SIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    April 25, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    SIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    HILI HAPA DAU LA KUMPATA COLE PALMER

    TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI TAREHE 25.4.2025

    PRESHA YA KUUKOSA UBINGWA YATAWALA REAL MADRID

    TAREHE PAMOJA NA UWANJA AMBAO DABI YA KARIAKOO ITAPIGWA

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.