Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » “Reece James ni beki bora zaidi wa kulia Duniani”-Rosenior.
    KIMATAIFA

    “Reece James ni beki bora zaidi wa kulia Duniani”-Rosenior.

    ChikaoBy ChikaoMarch 15, 202601 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Kocha mkuu wa Chelsea FC, Liam Rosenior, amesema klabu hiyo “imepata mchezaji bora zaidi duniani katika nafasi yake” baada ya beki wa kulia Reece James kusaini mkataba mpya wa miaka sita.

    James, mwenye miaka 26, alijiunga na timu kubwa ya Chelsea na kucheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa mwezi Septemba 2019 akitokea timu ya vijana ya ‘the blues’.

    Rosenior alisema hawezi kuacha kutabasamu kutokana na habari kwamba James ataendelea kubaki klabuni kwa muda mrefu, “Siwezi kuacha kutabasam Reece James amesaini mkataba mpya na tumehakikisha mchezaji bora zaidi duniani katika nafasi yake anaendelea kubaki hapa!”

    “Alikuwa na fursa nyingi za kuondoka katika klabu hii,” alisema Rosenior, ambaye alimrithi Enzo Maresca katika uwanja wa Stamford Bridge mwezi Januari”.

    “Sio tu kuhusu ukubwa na hadhi ya klabu aliyokulia, bali pia ni kuhusu imani na kujiamini kwake katika kile tunachokifanya na tunakotaka kufika. Tumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu hilo ,Kwa yeye kusaini mkataba na kuweka imani yake kwetu ni hatua kubwa sana.”Amesema Rosenior.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleBAJABER ARUDI KWENYE RAMANI KUPITIA WITO WA TAIFA
    Next Article VINARA LIGI DARAJA LA KWANZA RAHA TUPU

    Related Posts

    HILI HAPA DAU LA KUMPATA COLE PALMER

    April 25, 2026

    PRESHA YA KUUKOSA UBINGWA YATAWALA REAL MADRID

    April 25, 2026

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    April 17, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Wafungaji Bora Mapinduzi Cup 2026

    Mshindi lazima apatikane leo Yanga SC vs Simba SC, Muungano CUP

    IBENGE AKIRI KUTORIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    SIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    HILI HAPA DAU LA KUMPATA COLE PALMER

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.