Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » RUSHINE MKATABA MWINGINE SIMBA, ULINZI WAIMARIKA
    KITAIFA

    RUSHINE MKATABA MWINGINE SIMBA, ULINZI WAIMARIKA

    ChikaoBy ChikaoMarch 9, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    UONGOZI wa klabu ya Simba umefanikiwa kumuongezea mkataba beki wake tegemeo Rushine De Reuck baada ya kukamilisha taratibu zote za kipengele cha kuongeza muda kilichokuwapo kwenye makubaliano ya awali.

    Hatua hiyo inaashiria kuendelea kwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili huku uongozi wa timu ukionyesha imani kubwa kwa mchezaji huyo raia wa Afrika Kusini.

    Awali Rushine alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja ndani ya kikosi cha Simba uliokuwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine endapo pande zote zingekubaliana. Baada ya tathmini ya mwenendo wake uwanjani na mchango wake katika safu ya ulinzi, uongozi wa klabu umeamua kuamsha kipengele hicho na kumfanya aendelee kuitumikia timu hiyo.

    Imeelezwa kuwa beki huyo amekuwa mmoja wa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Simba tangu alipojiunga na klabu hiyo. Uwezo wake wa kusoma mchezo, kupiga mipira ya juu pamoja na uzoefu wake mkubwa umeifanya Simba kuwa na uimara zaidi katika safu ya nyuma.

    Mtoa habari huyo amesema hatua ya kumuongezea mkataba inatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kuimarisha kikosi chake kwa muda mrefu. Simba imekuwa ikifanya maboresho katika kikosi chake ili kuhakikisha inabaki kuwa na ushindani mkubwa katika mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa.

    “Rushein   amekuwa akionyesha kujitoa kwa kiwango kikubwa kila anapopewa nafasi ya kucheza. Nidhamu yake ndani na nje ya uwanja imekuwa mfano kwa wachezaji wengine na moja ya sababu zilizochangia kupewa nafasi ya kuendelea kusalia klabuni hapo,” amesema mtoa habari.

    Ameongeza kuwa  sasa kila kitu kimekamilika rasmi na beki huyo ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao. Hatua hiyo inaipa timu hiyo utulivu katika safu ya ulinzi huku ikijiandaa na malengo makubwa ya ushindani katika ligi na mashindano mengine.

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMAJERUHI YAWALAZIMISHA PEDRO KUBADILI KIKOSI YANGA
    Next Article KAGOMA ASEMA BADO ANA KAZI KUBWA SIMBA

    Related Posts

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.