KIMATAIFA
CONGO BRAZZAVILLE YAONDOLEWA CHAN
Congo Brazzaville imeondolewa kushiriki michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu.
Michuano hiyo itafanyikia nchini Kenya, Uganda na Tanzania katika tarehe ambazo bado hazijawekwa wazi.
Congo Brazaville waliokuwa Kundi D pamoja na Nigeria, Sudan na Senegal wnafasi yao imechukuliwa na Equatorial Guinea.
Kutolewa kwao kunafuatia madai kwamba walimchezesha mchezaji asiyestahili, mshambuliaji Japhet Eloi Mankou Nguembete.
Zaidi ya hayo Chama cha soka cha Congo Brazaville kimepigwa faini ya Dola za Kimarekani 10,000 ambayo inatakiwa kulipwa ndani ya siku 60.