KIMATAIFA

BALE: RONALDO HAKUNIZIDI KITU, JINA LANGU HAWALIPENDI

Akiwa kwenye mahojiano hivi karibu ni mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na Wales Gareth Bale anasema kama yasingekuwa majeraha angekuwa kwenye kiwango sawa na Messi na Ronaldo huku akisisitiza kuwa yeye alikuwa bora mazoezini kuliko Ronaldo.

“Kama isingekuwa majeraha, jina langu lingekuwa kwenye mjadala sawa na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi”

“Katika mazoezi ya Real Madrid, nilikuwa mpigaji bora wa free-kick, mmaliziaji bora, lakini Cristiano alipendelea kupiga mipira ya adhabu na faulo fupi zote isipokuwa kona. Lakini katika mazoezi, siku zote nilikuwa na asilimia kubwa ya kufunga mkwaju wa faulo kuliko yeye.

Related Articles

“Dhidi ya Liverpool kwenye fainali, nilifunga bao la kustaajabisha, lakini hakuna anayetaka kukiri kuwa lilikuwa bao bora katika historia ya Ligi ya Mabingwa kwa sababu tu jina langu ni Gareth Bale.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button