Manchester City wako tayari kumuuza mlinzi Kyle Walker, Bournemouth wanataka “pesa nyingi” kwa ajili ya beki Milos Kerkez na Liverpool wanatafuta mbadala wa Virgil van Dijk.
Manchester City wako tayari kumuuza nahodha Kyle Walker, 34, kwa takriban £15m msimu ujao wa joto. Beki huyo wa Uingereza analengwa na klabu ya Al-Ahli ya Saudi Arabia. (Daily Star)
Manchester City na Liverpool zinaonyesha nia ya kumnunua fowadi wa Brighton Muargentina Facundo Buonanotte, 19, ambaye yuko kwa mkopo Leicester City. (Fichajes – in Spanish)
Bournemouth itataka “pesa nyingi” ikiwa ni watilie maanani kumuuza beki wa Hungary Milos Kerkez, 20, ambaye anavutia Liverpool, Arsenal na Manchester United. (Football Insider)
Liverpool wamemlenga beki wa Borussia Dortmund na Ujerumani Nico Schlotterbeck, 24, kama mbadala wa Virgil van Dijk iwapo Mholanzi huyo ataondoka katika klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Caught Offside)
Arsenal wametiwa moyo iwapo wanataka kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo, 24, baada ya kusema yeye ni shabiki wa Gunners na anataka kucheza soka ya Ligi ya Mabingwa. (Football 365)
Manchester United huenda ikamsajili tena beki wa kushoto Alvaro Fernandez, 21, ambaye alijiunga na Benfica kwa mkataba wa kudumu msimu wa joto na anafuatiliwa na Liverpool na Real Madrid. (Teamtalk)
Barcelona wameanzisha mazungumzo ya mkataba kuhusu makubaliano mipya kwa mlinzi Ronald Araujo, 25 – anayelengwa na Manchester United na Chelsea – na kiungo Frenkie de Jong, 27, ambaye pia anasakwa na Red Devils. (90 min)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 31, anaonekana kutokuwa na uwezekano wa kuichezea tena Juventus mara tu marufuku yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli itakapokamilika mwezi Machi baada ya mkurugenzi wa klabu kusema kuwa kikosi kimekamilika bila yeye. (DAZN, via ESPN)
Meneja mpya wa England Thomas Tuchel atapokea marupurupu ya pauni milioni 3 ikiwa anaweza kuiongoza Uingereza kushinda Kombe la Dunia la 2026. (The Sun)