KIMATAIFA

ARSENAL YAVIONGOZA VILABU 5 KWENYE KUGOMBEA SAINI YA OMAR MARMOUSH

Kutoka Ligi ya Bundesliga ya Ujerumani, Fowadi wa klabu ya Eintracht Frankfurt, Omar Marmoush yuko kwenye rada za vilabu vikubwa vya Ligi kuu ya Uingereza ambavyo vinataka kupata huduma yake kwenye dirisha lijalo la usajili.

Maskauti kutoka timu kadhaa za Ligi hiyo wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo raia wa Misri.

Taarifa zinaitaja Arsenal kama klabu ya kwanza inayomtolea ‘udenda’ mchezaji huyo huku Chelsea, Liverpool na Manchester United pia zikionesha nia.

Magazeti mengi ya kimataifa yamesifu uchezaji mzuri wa nyota wa Misri.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button