Rashid Yazid, Msimamizi wa Kibu Denis amezungumza na Sokaleo.co.tz kwa mara ya kwanza tangu sakata la Kibu Denis kutowasili kambini kujiunga na timu kwenye maandalizi ya msimu, huku Timu yake ya Simba ikitoa taarifa kwa Umma jana kua imemalizana na mchezaji huku ikishangaa kwanini hajawasili kambini mpaka leo na akitoa sababu nyingi, pia ikisema kama klabu itatoa adhabu kwa utovu huo wa nidhamu.
Amesema “Kama mlivyoiona taarifa, klabu imekuwa confused kuhusu wapi alipo mchezaji. Siku tatu nyuma nilikosa mawasiliano na mchekeshaji, nikawa na maswali, viongozi wananiuliza yupo wapi mchezaji!”- Yazid
“Jana tumepata uhakika zaidi kuwa mchezaji yupo Ulaya. Jana ndio ameondoka airport, lakini Mimi nilikuwa najua yeye yupo Kigoma kwa matatizo ya kifamilia.”
“Mchezaji ameshawishiwa na ametoroshwa kwenda Ulaya, mchezaji hana ‘technical know how’ yeye ni mtaalamu wa mpira! ameshawishiwa na kufanya mipango ya kuondoka kwenda Ulaya.”
“Kilichotokea ni utovu wa nidhamu kwanza yeye kwenda Kigoma kwenda kumuuguza mzazi wake hakutoa taarifa kabla baadaye mimi niliitaarifu klabu juu ya suala la matatizo yake ya kifamilia…. Taarifa za kuuguliwa na mzazi alizitoa kwa kiongozi Simba ambaye sio sahihi.”
“Mimi ndiye ninayetambulika na Simba Sc, nimeanza kumsimamia kuanzia dili lake la kwanza Simba Sc, awali nilikuwa mwanasheria ya Kibu tu kabla ya Jamal (aliyekuwa wakala wake) kunikabidhi baada ya kuwa na majukumu mengine nje ya Nchi.”