Tasnia ya Michezo nchini Tanzania inaendelea kukua kwa kasi sana ambapo hii inaenda sambamba na uhitaji wa kupata habari kwa wadaau wanaofuatilia michezo pia umekuwa mkubwa sana, yote haya yanapelekea pia watoaji wa huduma hiyo ya habari pia kuongezeka, wapo wanaofanya vyema sana katika utoaji wa habari za kimichezo nchini Tanzania katika upande wa blog na website.
Leo nimekuletea blog 10 bora katika kutoa habari za kimichezo nchini Tanzania ambazo zimekuwa kivutio kwa watembeleaji wengilakini pia kwenye utoaji wahabari zenye uhakika na tena kwa wakati.
1: Soka Leo
Soka leo ni blog iliyoanza kutoa habari za kimichezo mwaka 2020, ambapo imekuwa blog ya kimageuzi kwa kuwa mstari wa mbele kwenye utoaji habari za kimichezo na ikiwa ni blog kisasa zaidi, lakini ikijikita pia kwenye michezo mbali mbali kama vile Boxing, Basketball nk, imeuwa ni blog yenye ushindani pia katika utoaji wa taarifa sahihi tena kwa wakati zote za Kitaifa na Kimataifa, sambamba na makala mbali mbali ya kimichezo na historia katika soka.
2: Mwanaspoti
Mwanaspoti ni moja kati ya kampuni ambayo ipo ndani ya mwamvuli wa Nation Media Group, kwa takribani miaka 14 Mwanaspoti imekuwa ni blog bora kwa wasomaji wa habari za kimichezo sambamba wakiwa na gazeti ambalo lina kauli mbiu isemayo kata kiu ya michezo na Burudani limekuwa ni gazeti bora kwa watanzania wapenzi wa michezo sambamba wakifanya vyema katika ulimwengu wa blog kwenye utoaji wa habari za uhakika na kwa uharaka.
3: Soka La Bongo
Soka la Bongo ni blog iliyoanzishwa mwaka 2020 May 15 ambapo imekuwa pia ikijihusisha kwenye utoaji wa habari za michezo pekee na imekuwa ni blog yenye ushawishi na ushindani kwenye blog nyingine mbalimbali za utoaji habari za kimichezo pekee.
4: Saleh Jembe
Saleh Jembe ni moja kati ya waandishi nguli wa habari za kimichezo nchini Tanzania ambapo kwenye ukuaji wa sekta ya mtandao walakini huwenda akaona kuwa ni bora kuja na platform hii ambapo kutokana na kuaminika kwake kwenye uchambuzi hiyo ikaamisha imani ya wadau wa soka katika blog yake hii bora kwa habari za michezo ambayo inafanya vizuri pia kwenye utoaji wa habari.
5: Bin Zubeiry
Bin Zubeiry ni moja kati ya blog kongwe nchini Tanzania kwenye utoaji wa habari za kimichezo pekee, imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka 2015 na imekuwa ikiaminika na watanzania ambao ni wapenzi wa habari za kimichezo.
6: Soka Tanzania
Soka Tanzania ni blog iliyoanza kufanya kazi mwaka 2023 ikiwa ni blog ambayo bado haina muda refu lakini imekuja na kuanza kuonyesha ushindani wake kwenye tasnia ya utoaji habari za kimichezo huku pia ikijizolea imani kwa watembeleaji wake kwa utoaji habari za uhakika na kwa uharaka.
7: Meridian Bet Sport
Meridian Bet Sport ni website ya kimichezo ambayo ipo chini ya mwamvuli wa kampuni ya kubashiri yaa MeridianBet huku kwa website hii ikianza kufanya kazi tangu mwaka 2020 April 19 imekuwa pia ikifanya vizuri lakini moja na sehemu iliyovutia wengi ni utoaji wake wa habari za kimataifa ambapo sio rahisi kwa blog nyingi za Tanzania zinatoa habari za michezo za kimataifa kwa wingi.
8: Tanzania Web
Tanzania Web kiuhalisi sio website ya michezo pekee inajihusisha na utoaji wa habari mbali mbali za kitaifa, burudani, Biashara nk, lakini tumekuwekea kiungo chake cha habari za michezo pekee ukibonyeza hapo juu na ni website pia ambayo inafanya vizuri sana kwenye utoaji habari za michezo na ikianzishwa mwaka 2024 January 8.
9: Global Publishers
Global Publishers nayo pia sio blog ya kutoa habari za michezo pekeyake ijapokuwa ni moja kati ya kampuni bora sana kwenye utoaji wa habari online na yenye kuaminika pia nchini Tanzania.
10: Dar24
Sambamba na Dar24 sio blog ya kutoa habari za kimichezo pekee nayo inajihususha na utoaji wa habari nyingine mbali mbali lakini ikifanya kazi tangu mwaka 2012 ikiwa ni moja kati ya media ya online kubwa nchini na ikifanya vizuri katika utoaji wa taarifa mbali mbali.