KITAIFA

YANGA YATOA TAMKO BAADA YA MECHI KUTOFANYIKA, WAPEWE USHINDI, BODI IVUNJWE

Sakata la kuahirishwa kwa mchezo wa Derby ya Kariakoo limeingia sura mpya baada ya Kamati ya Utendaji wa Yanga Sc katika kikao chake cha Machi 9, 2025 kutoa msimamo wake kuhusu uamuzi huo wa Bodi ya Ligi kuahirisha mechi hiyo huku ikitoa pole kwa Wanachama, Mashabiki, Wapenzi na wadau wa mchezo wa mpira wa miguu waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na kushindwa kushuhudia mechi hiyo.

Kamati ya Utendaji ya Yanga Sc imeitaka Bodi ya Ligi kuipa klabu hiyo haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi. Katika hatua nyingine Kamati ya Utendaji ya Yanga Sc imekubaliana kutoshiriki mchezo namba 184 kwa tarehe yoyote itakayopangwa.

Vilevile kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, Klabu ya Yanga imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo.

Hivyo klabu hiyo imeliomba Shirikisho la Mpira wa miguu (TFF) kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wengine waadilifu na wenye nia njema kwa maslahi mapana ya mpira wetu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button