WACHEZAJI WANAOONGOZA KWA HAT TRICK MSIMU WA 2024/25 NBC PREMIER LEAGUE

NDANI ya Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika kuna wakali wakucheka na nyavu ambao wameandika rekodi zao za kusepa na mipira Bongo msimu wa 2024/25.
Nyota wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi ni Prince Dube ambaye yupo ndani ya kikosi cha Yanga huyu alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa, Uwanja wa KMC Complex waliposhuhudia ubao ukisoma Yanga 3-2 Mashujaa.
Yanga ni namba moja kwenye eneo la kucheka na nyavu Bongo ambapo safu ya ushambuliaji imetupia mabao 58 na pointi zao kibindoni ni 58 ikiwa inaongoza ligi.
Mkali wa pili kucheka na nyavu akiwa na hat trick ni Aziz Ki ambaye huyu alifunga kwenye mchezo dhidi ya KMC walipoibuka na ushindi wa mabao 6-1 Uwanja wa KMC Complex.
Yanga hat trick zote zimekusanywa Uwanja wa KMC Complex ambapo mchezo mmoja dhidi ya Mashujaa walikuwa nyumbani na mchezo mwingine dhidi ya KMC walikuwa ugenini.
Nyota mwingine ni Steven Mukwala huyu wa Simba alifunga mbele ya Coastal Union, Machi Mosi 2025 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ubao uliposoma Coastal Union 0-3 Simba.
Kituo kinachofuata ni Machi 8, Yanga v Simba, Uwanja wa Mkapa wakali hawa wanatarajiwa kukutana msako wa pointi tatu.