Samuel Eto’o Nyota Inayoendelea Kung’aa Kwenye Historia ya Soka.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Cameroon ambaye kwa sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon Samuel Eto’o anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee katika historia ya soka kushinda ‘Treble’ makombe matatu makubwa akiwa na vilabu viwili tofauti katika misimu miwili mfululizo.
Eto’o aliweka rekodi hiyo msimu wa 2009/10 akiwa na Inter Milan huku akifanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya,Ligi Kuu ya Italia Serie A na Kombe la Coppa Italia ikiwa alitoka kushinda Makombe matatu akiwa na Barcelona msimu wa 2008/09 baada ya kutwaa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya,Ligi Kuu Hispania Laliga na Kombe la Copa del Rey.
Nguli huyo pia bado anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa miongoni wa wachezaji bora wa muda wote wa bara la Afrika baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010.
Eto’o alistaafu kucheza soka la kulipwa mwaka 2019 alipokuwa na umri wa miaka 38 huku akiwa amefunga magoli 427 pasi za magoli 136 akiwa mchezaji pekee wa Afrika aliyewania tuzo za Ballon D’or mara nyingi zaidi licha ya kuwa hajawahi kutwaa tuzo huyo.
Mshambuliaji huyo wa muda wote wa Mashindano ya AFCON leo anasherekea kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka 44.
Kipi unakimbuka zaidi kwa Mwamba huyu ?.