KITAIFA

HUYU HAPA MKALI ZAIDI KWA KUCHEKA NA NYAVU BONGO

KIUNGO wa kazi ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Jean Ahoua ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika akiwa katupia mabao 12.

Ushindi wa mabao 6-0 waliopata dhidi ya Dodoma Jiji, Machi 14 2025 unampa nafasi yakufikia mabao hayo kwa kuwa alitupia mabao mawili huku mawili yakifungwa na Kibu Dennis ambaye alifungua akaunti ya mabao baada ya kuyeyusha miezi 16 bila kufunga kwenye ligi.

Bao jingine lilifungwa na Ellie Mpanzu ambaye anafikisha mabao matatu kwenye ligi na Steven Mukwala bao moja akifikisha mabao 10 ndani ya ligi huku Ahoua akiwa namba moja kwenye chati.

Related Articles

Rekodi zinaonyesha kuwa ni mechi 21 alipata nafasi ya kucheza akitupia mabao 12 ni pasi za mabao 6 katoa na kumfanya ahusike kwenye mabao 18 kati ya 52 yaliyofungwa na Simba kwenye ligi.

Ni dakika 1,550 kakomba uwanjani akiwa na wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 86. Kwenye mabao hayo 12 aliyofunga ni mabao matano kafunga kwa penati na yote kafunga kwa mguu wa kulia.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button