KITAIFA

AZIZ KI HATIHATI KUIKOSA DABI, KOCHA ASHUSHA PRESHA

KUELEKEA Kariakoo Derby, Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 58 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 22 wanatarajiwa kumenyana na Simba iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza jumla ya mechi 21 kwenye ligi.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga, pointi tatu zilielekea Jangwani kwa wababe hao ambao safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao 58.

Hamdi amesema: “Ni matumaini yangu kuwa kesho tutafanya vizuri. Tumefanya maandalizi makubwa ya kutosha kuhimili presha ya Derby. Hatuna wasiwasi na maandalizi yetu, kilichobaki ni kwenda kufanyia kazi kile ambacho tumeandaa kwenye uwanja wa mazoezi.

“ Tunaheshimu sana wapinzani wetu, lakini lazima ukweli uwekwe wazi kuwa sisi ni timu bora. Natarajia kuona mchezo wa kimbinu sana, timu zote zina nguvu, timu zite zina dhamira ya kushinda mchezo unaokuja. Nadhani mchezo utakuwa wazi sana kwani kila timu inajiamini.

“Tunatarajia kuona mchezo ambao kila mtu atapambana kwa kila namna. Niseme tu sisi tupo tayari na tupo imara kwa mchezo huo. Wachezaji wote wapo fiti kujiandaa na mchezo, mchezaji pekee ambaye nina wasiwasi nae ni Aziz Ki ambaye alipata shida ya mgongo.

“Siwezi kusema kama atakuwepo au hatakuwepo bado ni 50/50 nafikiri mpaka kesho nitakuwa na majibu sahihi. Hii sio Derby yangu ya kwanza, nimewahi kucheza Derby ambayo ilikuwa na mashabiki tarkibani 120,000.

“Siwezi kuwa na presha. Isipokuwa tu naheshimu wapinzani wangu, nasubiri tu mchezo mzuri na wa kuvutia. Mashabiki waje kupata burudani wasiwe pia wasije na presha.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button