Tems na Ayra Star walishuhudia Arsenal akipasuka dhidi ya Westham.

Wanamuziki staa wa kike kutoka Nigeria Tems na Ayra Star walihudhuria Mechi ya EPL Arsenal akiwa Nyumbani katika uwanja wa Emirates Stadium dhidi ya West Ham ambapo walipasuka 1-0 na kushindwa kupata alama tatu muhimu na kuwafanya Liverpool kuzidi kujihakikishia nafasi ya kuuchukua Ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.
TheRadar – How Ayra Starr, Tems are changing narrative about ‘female friendship’ in Nigerian music industry
Ambapo wanamuziki hao walipata pia nafasi ya kupiga picha na Bukayo Saka ambaye hakuweza kucheza mchezo huo kutokana na majeraha yanayo msumbua lakini pia wakiondoka na jersey yake yenye namba 7 mgongoni
Hii imetokea mara baada ya Tems kutangazwa kama mshiriki mwenza kwenye moja ya football Club huko Marekani (San Diego FC).