KITAIFA

Nyota wa Tanzania ashikiliwa na Polisi Uganda ahusishwa na kifo cha mchezaji wa Vipers

Polisi nchini Uganda wanamshikilia mchezaji wa kimtaifa wa mpira wa kikapu wa Tanzania Naima Omary, kwa tuhuma za kuhusishwa na kifo cha kusikitisha cha Abubakar Lawal, mshambuliaji wa Nigeria wa Vipers SC, aliyefariki siku ya Jumatatu kwa kudaiwa kuanguka kutoka ghorofa ya tatu katika Kituo cha Biashara cha Voice Mall huko Bwebajja, kando ya Barabara ya Entebbe, jijini Kampala Uganda.

Naima, anayeaminika kuwa mtu wa mwisho kuwa na Lawal kabla ya kifo chake, kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kajjansi Wilaya ya Wakiso huku uchunguzi ukiendelea.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni, polisi walieleza kwa kina mazingira ya tukio hilo.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye alifika Voice Mall kwa gari lake, nambari ya usajili UBQ 695G, aliripotiwa kumtembelea Naima, ambaye alikuwa akikaa katika chumba namba 416 tangu Februari 20, 2025.

Naima, ambaye alikuwa mchezaji na mwanafunzi wa St. Mary’s Kitende kwa ufadhili wa masomo ya mpira wa kikapu kutoka Tanzania alikuwa nchini Uganda kwa ridhaa ya wazazi wake, awali ili kuendeleza taaluma yake ya mpira wa kikapu.

Kwa mujibu wa taarifa yake, raia huyo wa Tanzania alisema aliondoka na kumuacha Lawal chumbani akiandaa chai ndani ya chumba hicho na kutoka nje kwenye jengo lililokuwa karibu na eneo hilo.

Muda mfupi baadaye, karibu saa 8:00 asubuhi, Lawal alianguka kutoka kwenye balcony na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Entebbe, ambako alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Polisi walisema walipata vitu kadhaa vya kibinafsi kutoka kwa mkoba mweusi wa Lawal, ikiwa ni pamoja na simu mbili za kisasa, jozi ya viatu vya wazi, vifaa vya sauti, seti ya mafunzo na chaja.

Familia ya Lawal imeomba mwili wake urejeshwe Nigeria, na Rais wa Vipers SC Dkt. Lawrence Mulindwa aliahidi kusaidia katika mchakato huo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button