KITAIFA

FADLU ATUMA UJUMBE MZITO KWA TABORA UNITED

FADLU ATUMA UJUMBE MZITO KWA TABORA UNITED

FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Tabora United utakuwa na ushindani mkubwa lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa KMC, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 3-0 Tabora United huu ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa wababe hawa kukutana uwanjani.

Mchezo uliopita Simba ilicheza kwenye CRDB Federation Cup ilipata ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Kilimanjaro Wonders.

Related Articles

Kocha huyo amesema: “Kwetu ni mchezo muhimu na tunawaheshimu wapinzani wetu kutokana na uimara ambao wanao lakini tupo tayari kwa ajili ya kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu.”

Ofisa Habari wa Tabora United, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanaamini watapambana kupata pointi tatu.

Tayari kikosi cha Simba kipo Tabora kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Februari 2 2025.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button