KITAIFA

AZIZ KI AMESHINDIKANA, NDOA SIO KIKWAZO CHA KUWAPA FURAHA WANANCHI

AZIZ Ki ambaye alianzia benchi kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji, Uwanja wa CCM Kirumba amepachika mabao mawili kati ya matatu waliyonayo Yanga.

Ubao umesoma Pamba Jiji 0-3 Yanga, Shadrack Boka alipachika bao la ufunguzi dakika ya 28 kwa pigo la faulo ni pointi tatu mali ya Yanga ambayo dakika 45 za mwanzo walikuwa wakishambuliwa zaidi na Pamba Jiji.

Djigui Diarra dakika 45 za mwanzo alikuwa kazini kupambana kuokoa hatari za Pamba Jiji ambao walipiga mashuti matatu yaliyolenga lango yakakutana na mikono ya Diara ambaye ni mchezo wake wa 16.

Aziz Ki amepachika mabao mawili ndani ya dakika moja ilikuwa dakika ya 75 na 76 akifikisha jumla ya mabao 7 ndani ya ligi msimu wa 2024/25.

Yanga inakuwa imefunga jumla ya mabao 58 kwenye ligi wakiwa vinara na pointi 58. Kwenye mchezo wa leo Yanga walipiga kona 7 ambapo katika hizo sita zilipigwa na Maxi Nzengeli na moja ni Aziz Ki huku Pamba Jiji wao wakipiga kona sita.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button