KITAIFA

YANGA WATUPA DONGO KIMTINDO UNYAMANI ISHU YA KIMATAIFA

“Kuna timu ambayo ipo kwenye mashindano na ina pointi 9 inaweza isitinge hatua ya robo fainali,” moja ya kauli ya Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe ikiwa ni kama dongo kimtindo kwa Simba amba oni watani zao wa jadi.

Ikumbukwe kwamba Simba inapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kucheza mechi nne imekusanya pointi 9 lakini sio wao pekee hata vinara kwenye kundi hilo Constatine nao wana pointi 9 kibindoni kutoka kundi A.

Yanga ipo Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kucheza mechi nne kutoka kundi A imekusanya pointi nne ikiwa nafasi ya tatu ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe.

Yanga imefunga mabao manne na yote ni dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa kwanza ugenini walipata sare ya kufungana bao 1-1 na  mchezo wa pili uliokamilisha dakika 180 Uwanja wa Mkapa ilikuwa Yanga 3-1 TP Mazembe.

Hivyo ni pointi nne Yanga imekomba mbele ya TP Mazembe kwa kuwa mechi zake mbili za mwanzo ilipoteza ina kibarua cha kulipa kisasi kwenye mechi zijazo kusaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Kamwe amesema: “Tunatambua tuna mechi ngumu mbele yetu lakini hesabu kubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo na hilo linawezekana kikubwa ni utayari na wachezaji wanatambua kwamba kuna kazi kubwa watapambana na mashabiki tujitokeze kwa wingi.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button