KITAIFA

TUTACHUKUA USHINDI KUTOKA KWA SIMBA NA YANGA

Kocha wa Azam, Rachid Taoussi amesema licha ya kudondosha pointi nyingi duru la kwanza ana nafasi ya kuipambania timu hiyo kutwaa taji msimu huu, huku akidai wazi kuwa ana pointi sita kwa Simba na Yanga.
.
Azam ipo nafasi ya tatu katika msimamo baada ya kukusanya pointi 36 ikiwa mbele mchezo mmoja dhidi ya Simba (40) na Yanga (39) ambazo pia zimemuacha.
.
“Kudondosha pointi mzunguko wa kwanza haina maana tumeshakata tamaa. Bado tuna nafasi na ukizingatia washindani wetu tuna mechi nao mzunguko huu wa pili hatuwezi kufanya makosa kudondosha tena dhidi yao hasa kwa Simba ambayo ilitufunga mzunguko wa kwanza,” alisema.
.
“Ukitaka kushinda taji usikubali kuwa mnyonge mbele ya mshindani wako, pointi nne ambazo wapo mbele yetu vinara wa ligi tatu tutazichukua kwao na upande wa mabingwa watetezi pia ambao wanapambania kutetea taji lao tutahakikisha tunaendelea tulipoishia.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button