KITAIFA

SAIDO ATOA MASHARTI YA KUTUA KENGOLD

Wakati mabosi wa KenGold wakipigia hesabu za kumsainisha aliyekuwa kiungo wa Yanga na Simba, Mrundi Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, nyota huyo ameweka masharti mapya kwa viongozi wa timu hiyo ya jijini Mbeya ili akaitumikie kwa miezi sita.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo, zinaeleza ‘Saido’ anahitaji pesa ya usajili Sh50 milioni na mshahara wa Sh12 milioni kwa mwezi, ingawa viongozi bado hawajafikia makubaliano rasmi juu ya kiasi hicho cha fedha anachokihitaji.

“Kwenye pesa ya usajili sio ishu sana ingawa mshahara ndio changamoto kwa sababu viongozi wanataka wampe Sh4 milioni na hii ni kutokana na kutocheza kwa muda mrefu, bado wanaendelea na mazungumzo juu ya suala hilo,” kilisema chanzo changu

Chanzo hicho ambacho kiliomba kuhifadhiwa jina lake, kilisema viongozi wanaamini uwezo wa mchezaji huyo kwa kushirikiana na nyota wengine, utaleta chachu ya kukinusuru kikosi hicho na janga la kushuka daraja hivyo wanapambana kuinasa saini yake.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button