NILIMPA 13M AKADAI NDOGO, NILITAMANI KURUDISHA MUAMALA
Victor Osimhen anasimulia namna alivyomsaidia rafiki yake wa utotoni kiasi cha pesa lakini hakuonekana kukithamini.
Osimhen anasema: “Nilikuwa nikituma pesa kwa rafiki yangu mmoja wa utotoni, lakini siku moja, aliniambia kuhusu biashara anayotaka kuanzisha na alihitaji usaidizi wa kifedha. Nilimtumia €5k(zaidi ya Sh mil 13) lakini hakuithamini na hata akaniambia alisoma kwenye habari kwamba napokea mshahara euro milioni 1 kila wiki, na alitarajia kama ningempa euro 50k (zaidi ya Sh mil 130) kuanzisha biashara hii nilikasirika sana. Nilitaka kurudisha muamala lakini sikuweza.
“Pesa hizo €5k zinaweza tu kununua pea moja ya viatu huko Ulaya, lakini nchini Nigeria ni pesa nyingi. Hakuna aliyenitumia dola 1 kabla sijaja Ulaya, nilihangaika usiku na mchana, na niliuza maji ya chupa mitaani. Watu wanapaswa kujifunza kuthamini chochote wanachopata kama zawadi, wasiwe na hisia hii ya kustahiki.”