KITAIFA

KOCHA RAMOVIC AFUNGUKA KILICHOMKWAMISHA IKANGALOMBO

Kikosi cha Yanga juzi kilishuka uwanjani na kuifumua Copco katika mechi ya Kombe la Shirikisho, huku mashabiki wakiachwa njia panda baada ya kumkosa uwanjani winga wao mpya Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’, hata hivyo imefichuka sababu zilizomzuia nyota huyo kushindwa kucheza.

Kocha wa Yanga Sead Ramovic amesema; “asingeweza kucheza kwa vile alipata homa kali karibu wiki nzima hii jana ndio ameanza kuwa sawa hakukuwa na ulazima kumlazimisha kucheza hii mechi (dhidi ya Copco),” alisema Ramovic na kuongeza;

“Tutamwona maendeleo yake zaidi Jumatatu (leo) tutakapoendelea na mazoezi, hajafanya mazoezi sawasawa na timu nzima tangu amefika na sasa amepata hiyo shida ya afya.

“Kuna kazi tunatakiwa kuifanya kwake (Ikanga), huyu ni mchezaji mpya ambaye alifika hapa tukiwa kwenye mechi ngumu za Ligi ya Mabingwa Afrika, tunataka kwanza kumuona na utayari wake kwa aina ya falsafa ya soka tunalotaka hapa,” alisema Ramovic.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button