KIMATAIFA

KASAINI MKATABA MGUMU WA UHUSIANO NA MPENZI WAKE

PRODIGY Endrick ambaye ni mchezaji chipukizi wa Klabu ya Real Madrid, akiwa na umri wa miaka 19, ameshika vichwa vya habari baada ya kuweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake Gabriely Miranda, 23, wameandikiana mkataba wa mahusiano yao, ambao umeonekana kuwa na masharti ya kipekee.

Endrick aliyasema hayo wakati akikipiga Palmerias ya Brazil akiwa na mpenzi wake katika mahojiano katika Podcast ya “Pod Delas” ambapo miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na:-

1: Marufuku kuonyesha mabadiliko makubwa ya kitabia pamoja na uraibu, pia ni lazima kusema neno “Nakupenda” katika hali zote.

2: Pande zote mbili haziruhusiwi kubishana katika maeneo ya umma (hadharani).

3: Pande zote mbili haziruhisiwi kuwa na uhusiano wa kimapenzi au wa karibu na watu wengine, wakiwemo wapenzi wao wa zamani.

4: Endapo mmojawapo atakiuka masharti hayo atalazimika kutoa faini kwa njia ya zawadi.

Hata hivyo Kocha wa Palmeiras, Abel Ferreira, alizungumzia suala hilo katika mkutano na waandishi wa habari kabla Endrick hajatua Madrid akisema: “Natumai (Endrick) ataendelea kuzingatia soka na hatababaishwa na mambo mengine. Ikiwa unataka kufikia viwango vya juu, lazima uzingatie kile ambacho ni muhimu.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button