AMWACHA MPENZI WAKE BAADA YA KUAMBIWA WAOANE
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Nigeria Victor Boniface anayeichezea Bayer Liverkusen ya Ujerumani imeripotiwa kuwa ameachana na mpenzi wa Rikke Hermine Raia wa Norway baada ya kudumu nae kwa miaka minne.
Sababu za Victor kuachana na Rikkie ni kutokana na mrembo huyo kushinikiza wafunge ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga nae ndoa ila kwa sharti la kusaini prenup.
Prenup ni Mkataba wa kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana (talaka) kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo.
Wanasoka wengi wamefilisika Duniani kutokana na kupeana talaka na wake zao wakiwemo Brown wa Man United, Louis Saha wa Man United na Emmanuel Eboue wa Arsenal.