YANGA YAKOMBA TATU ZA PRISON, BACCA, DUBE, MZIZE, WATUPIA
UBAO wa Uwanja wa KMC, Complex umesoma Yanga 4-0 Tanzania Prisons ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mabao ya Clement Mzize dakika ya 13, Ibrahim Bacca dakika ya 42, 83 na Prince Dube dakika ya 45. Kwenye mchezo wa leo Bacca amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Rekodi zinaonyesha kuwa katika mechi tano zilizopita wababe hawa waligawana pointi mara moja tu ilikuwa Yanga 0-0 Tanzania Prisons.
Yanga ilipata ushindi katika mechi nne ilikuwa Yanga 1-0 Prisons, Prisons 0-2 Yanga, Prisons 1-2 Yanga na Yanga 4-1 Prisons.
Yanga ilisepa na ushindi katika mechi nne huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 9 ndani ya mechi hizo ikifungwa mabao mawili.
Hivyo huu ni mchezo wa sita ambapo Yanga imecheza na Prisons kwenye ligi hivi karibuni ikiibuka na ushindi mara tano na kufunga jumla ya mabao 13.