KITAIFA

AHMED ALLY ATAMBA NA USAJILI WA SIMBA

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ameweka wazi kuwa usajili wao mpya wa Ellie Mpanzu umejibu kwa haraka licha ya kuwa na mchezo mmoja wa ushindani.

Nyota huyo mchezo wake wa kwanza ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar ambapo kwenye mchezo huo alikomba daika 57 alikuwa na uwezo wa kupiga mashuti ya mbali na spidi ndani ya uwanja.

Katika mchezo huo uliochezwa Desemba 21 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 2-5 Simba ukiwa ni ushindi mkubwa kupatikana ndani ya msimu wa 2024/25.

Ally amesema hakuna ambaye anaubeza uwezo wa Mpanzu kutokana na mwanzo alioanza nao atafanya makubwa ndani ya Simba.

“Unaona ni mchezo wake wa kwanza hana ugeni kwa kuwa anacheza kwa umakini na tayari ameshayazoea mazingira ya Tanzania kwa kuwa alikuwa hapa kwa muda mrefu balaa lake linazidi kukua kila leo.

“Sio kazi rahisi lakini kila mmoja anaona namna ambavyo wahezaji wanapambana kwenye mechi zetu, muhimu ni kupata pointi tatu kwenye mechi ambazo tunacheza.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button