KITAIFA

YAO YAO ANATAFUTIWA MBADALA YANGA

Gazeti la Mwanaspoti limeandika Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema Gamondi amewasilisha ripoti yake ya awali akitaka kuongezwa kwa wachezaji watatu katika dirisha lijalo la usajili akitaka kuletewa mshindani sahihi wa beki wa kulia Yao Akouassi.

Mbali na Yao nafasi hiyo inatumikiwa na Kibwana Shomari ambaye muda mrefu amekuwa akishangilia jukwaani akiwaachia beki na nahodha wake msaidizi Dickson Job na hata Denis Nkane kutumiwa eneo hilo kwa nyakati tofauti.

Licha ya Yao kuwa chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Gamondi, msimu huu beki huyo ameanza taratibu kukosa baadhi mechi zikiwemo tatu za Ligi Kuu Bara kutokana na kuwa majeruhi hatua ambayo imeanza kumshtua makocha na mabosi wa timu hiyo.

Katika mechi mec saba ambazo Yanga imecheza msimu huu. Yao ametumika kwa dakika 340 ambapo ni moja pekee dhidi ya Simba ndiyo amemaliza dakika zote tisini, zingine akifanyiwa mabadiliko.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button