KITAIFA
Yanga yaangukia kwa TP Mazembe na Al Hilal
Wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika, klabu ya Yanga imepangwa Kundi A lenye timu vigogo wa Soka la Afrika.
Yanga SC imepangwa na timu za TP Mazembe ya Congo DR, MC Algers ya Algeria na Al Hilal ya Sudan kusini.
Droo hiyo imechezeshwa mchana wa leo na Shirikisho la Soka Afrika CAF nchini Misri katika Jiji la Cairo.