Manchester United wanajiandaa kumnunua Randal Kolo Muani, Real Madrid wanamlenga William Saliba wa Arsenal, huku Chelsea wakimtaka Victor Osimhen.
Manchester United wameandaa ofa ya pauni milioni 58.6 kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 25 Randal Kolo Muani. (Fichajes, via Teamtalk)
Real Madrid wanataka kumsajili beki wa Arsenal na Ufaransa William Saliba mnamo 2025, huku Los Blancos wakiwa tayari wanawasiliana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Le 10 Sport – kwa Kifaransa)
Galatasaray watajaribu kuufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen kutoka Napoli kuwa wa kudumu, huku Chelsea wakiendelea kumsaka. Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atagharimu pauni milioni 68 mwezi Januari au pauni milioni 63 msimu ujao. (Corriere dello Sport – kwa Kiitaliano)
Manchester City wanamtaka kipa wa Porto Diogo Costa, 25, kama mbadala wa Ederson, lakini mlinda lango huyo wa Ureno atagharimu £63m. (Caught Offside)
Manchester United wamemfanya beki wa Chelsea Ben Chilwell, 27, kuwa kipaumbele yao katika usajili wa Januari. (Team Talk)
Kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi amesisitiza nia yake ya kusalia Real Sociedad licha ya tetesi zinazomhusisha na Manchester City. (Kioo)
Crystal Palace itaongeza kasi katika juhudi za kumsaka mshambuliaji wa Hammarby wa Ivory Coast Bazoumana Toure, 18, ambaye pia anawindwa na Manchester United na Celtic. (Give Me Sport)
Arsenal bado inamtafuta kiungo mshambuliaji katika usajili la Januari, licha ya mwanzo mzuri wa msimu uliofanywa na Mjerumani Kai Havertz, 25. (Football Insider)
Beki wa Liverpool Virgil van Dijk, 33, ndiye anayefuata katika orodha ya kusaini mkataba mpya baada ya klabu hiyo kufikia mustakabali wa muda mrefu wa beki wa Ufaransa Ibrahima Konate, 25. (Teamtalk)
Arsenal, Tottenham na Newcastle United wanavutiwa na kiungo wa kati wa Aston Villa na England Jacob Ramsey mwenye umri wa miaka 23. (Give Me Sport)
Newcastle huenda ikamuuza mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 32, mwezi Januari ili kumnunua mshambuliaji mpya. (Football Insider)
Marseille wamepiga hatua katika juhudi za kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 31, ambaye anaweza kucheza tena kuanzia Machi baada ya kupigwa marufuku kwa miaka minne kwa kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli kupunguzwa hadi miezi 18. (Mirror)
Pogba atakatizwa kandarasi yake na Juventus kufuatia marufuku yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli. (Fabrizio Romano)