Manchester United kuamua mustakabali wa Erik ten Hag, Liverpool na Newcastle zinazovutiwa na wachezaji wa Bundesliga na Bayern Munich wamepanga kutoa kandarasi ya pauni 400,000 kwa wiki.
Mustakabali wa Erik ten Hag, 54, kama kocha wa Manchester United utaamuliwa katika mkutano wa klabu siku ya Jumanne, huku msaidizi wake, Ruud van Nistelrooy, 54, akipendekezwa kushikilia nafasi hiyo kwa muda iwapo mabadiliko yatafanywa. (Guardian)
Manchester United wanavutiwa na Mjerumani Thomas Tuchel, 51, kama mbadala wa Ten Hag. (Manchester Evening News)
Mholanzi Ten Hag anaamini kuwa wakuu wake Manchester United wana imani naye kuelekea mapumziko ya kimataifa. (ESPN)
Liverpool wanavutiwa na mshambuliaji wa Eintacht Frankfurt na Misri Omar Marmoush, 25. Nottingham Forest na Aston Villa zilitaka kumsajili msimu uliopita. (Sky Germany – kwa Kijerumani)
West Ham wanatarajiwa kutoa bei ya kiungo wao wa kati kutoka Ghana Mohammed Kudus, 24. Liverpool, Arsenal, Manchester City na Chelsea wameonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Football Insider)
Newcastle inapania kumsajili winga wa Ujerumani Leroy Sane, 28, msimu ujao wa joto, mkataba wake utakapokamilika Bayern Munich. (Football Insider)
Bayern Munich wako tayari kumfanya mchezaji wa Ujerumani Jamal Musiala kuwa mchezaji wao anayelipwa kitita kikubwa, pamoja na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, kwa pauni 400,000 kwa wiki. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 hajadokeza kufanya mazungumzo na Real Madrid au Manchester City. (Sky Germany – kwa Kijerumani)
Wolves wanadumisha uungwaji mkono wao kwa kocha mkuu Gary O’Neil, 41, baada ya kumfukuza kocha Jack Wilson. (Sky Sports)
Barcelona wanamfuatilia mshambuliaji wa Lille na Canada Jonathan David, 24. (Todofichajes – kwa Kihispania)