MECHI TANO KELVIN JOHN YUPO BENCHI
MECHI tano mfululizo za mwisho ilizocheza Aalborg BK ya Denmark anayoichezea Mtanzania, Kelvin John zimemuweka benchi.
Hadi sasa chama la nyota huyo linaloshiriki Ligi daraja la kwanza limecheza mechi 13 ikiwa nafasi ya tisa kati ya 12 zinazoshiriki ligi na pointi 14 likishinda mechi nne, sare mbili na kupoteza saba.
Mara ya mwisho mshambuliaji huyo kuanza kwenye kikosi hicho Septemba 19 timu yake ikishinda mabao 4-1 dhidi ya Fredericia, John akifun-ga mabao mawili.
Baada ya kucheza dakika 90 ikiwa za kwanza tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu Septemba 23 timu hiyo ikacheza dhidi ya FC Copenhagen ikipoteza kwa 2-0 na John akiwa benchi.
Tangu hapo amekuwa akisugua benchi na mechi ya mwisho timu hiyo imecheza Oktoba 25 dhidi ya Silkeborg ikitoa sare ya 1-1 Mbappe huyo wa Bongo akicheza kwa dakika tano.
Hata hivyo John anakutana na changamoto hiyo ya namba mbele ya mshambuliaji Mathias Jor-gensen raia wa Denmark ambaye ndio ingia toka kwenye kikosi hicho. Mpinzani wa Mtanzania huyo ana mabao sita kwenye mechi 13.