MANGUNGU: TUNAELEKEA HATUA ZA MWISHO ZA MABADILIKO, MAUMIVU NI LAZIMA

“Tunakushukuru Rais wa Simba, Mohammed Dewji kwa hotuba nzuri. Pamoja na kusisitiza wanachama na wapenzi wa Simba kwenda viwanjani kuiunga mkono timu yao kadhalika tunawasisitiza sana umuhimu wa kutumia bidhaa zinazotokana na wadhamini wetu.”
“Tunafikia hatua ya mwisho ya mabadiliko lakini mabadiliko yoyote lazima yatakuwa na maumivu nadhani tuvumilie ili tumalize haya yote kwa pamoja.”
“Sisi bodi tutaunga utekelezaji wa mradi wa miundombinu. Mwisho nitoe shukrani kwa serikali, tunasafiri nchi mbalimbali na maafisa wa ubalozi wamekuwa wakija tunashirikiana ili kila kitu kwenda vizuri. Sisi Simba Sports Club tutaendelea kuunga mkono serikali.”- Murtaza Mangungu akizungumza katika mkutano mkuu wa Simba 2024.