Sio siri tena kuwa Bayern Munich inamtaka beki wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz huku Leverkusen ikiweka wazi ingependelea zaidi kumuuza mchezaji huyo nje ya Ujerumani ili kuepuka kuimarisha kikosi cha wapinzani wao.
Kwa mujibu wa Sky Germany, Manchester City nayo inamuona Wirtz kama chaguo sahihi la kuvaa viatu vya Kevin De Bruyne iwapo atahamia Saudi Arabia msimu ujao kwakuwa klabu ya Al-Nassr ya Cristiano Ronaldo imeonesha nia ya kumnunua.
Mbali na Man City na Bayern, vigogo wengine wa Premier League kama vile Liverpool, Arsenal, na Manchester United wameripotiwa kuonesha nia ya kutaka huduma ya mchezaji huyo.
Wirtz ameibuka kuwa mmoja wa wachezaji wanaowaniwa sana katika soka la Ulaya.