Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) limefikia uamuzi wa kucheza Mchezo wao wa nyumbani wa kutafuta kufuzu AFCON dhidi ya Timu ya Taifa la Cameroon bila ya uwepo wa Mashabiki ndani ya Uwanja.
Hilo linakuja baada ya Mashabiki wa Uganda kuonekana wakijaa katika Uwanja wa Namboole kwa nia ya kushangaa na kushabikia mastaa wa Timu ya Taifa la Cameroon haswa Golikipa wa Manchester United, Andre Onana.
Awali Kenya ilipanga kuacha kutumia Uwanja huo na kutaka kuhamia Uwanja wa Amahoro uliopo Rwanda jambo ambalo halikuafikiwa na kundi kubwa la viongozi wa (FKF).