KIMATAIFA
JE WAJUA: UTAMADUNI WA KUBADILISHANA JEZI ULIANZA MWAKA 1931
Utamaduni wa kubadilishana jezi ni wa muda mrefu katika soka.
Kumbukumbu zinaonyesha utamaduni huo kwa mara ya kwanza ulifanyika kwenye mechi ya Ufaransa dhidi ya England mwaka 1931.
Historia inaonyesha wakati huo Ufaransa na Uingereza zilikuwa na ushindani mkubwa kwenye mambo mbalimbali hata hivyo kwa upande wa soka Wafaransa walikuwa chini sana.
Katika mchezo huo wale waliokuwa wakionekana hawajui (Ufaransa) walishinda, kutokana na furaha waliyokuwa nayo walitaka kumbukumbu ya tukio hilo na hivyo kuwaomba wachezaji wa Kiingereza jezi zao na walipokubali ukawa ndio mwanzo wa utamaduni huo.