AZIZ KI, SAIDI USO KWA USO KUFUZU AFCON 2025
Nahodha wa timu ya taifa ya Burundi, Saidi Ntibazonkiza anatarajia kukiongoza Kikosi cha Burundi Intamba Murugamba katika kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Burkina Faso katika kusaka tiketi ya kuwania kufuzu AFCON 2025 nchini Morocco.
Kwa upande mwingine, Aziz KI atakuwa na kibarua kikubwa mbele ya Intamba Murugamba katika mchezo huo ambao utapigwa leo majira ya usiku katika uwanja wa Olympique Alassane Ouattara wenye uwezo wa kubeba mashabiki elfu 60.
Kwa upande wa Burundi watawakosa wachezaji muhimu katika kikosi cha timu ya taifa ambao ni Ndayishimiye Yousuf Nyange anayekipiga katika klabu ya Nice ya Ufaransa na Fredrick Nsabiyumva ambaye ana kadi mbili za njano.
Saidi Ntibazonkiza na Aziz Ki watakuwa wana jukumu kubwa katika kuviongoza vikosi vyao isitoshe pia waliwahi kucheza wote katika vilabu vikubwa nchini Tanzania za Yanga SC na Simba
SC.
Aziz KI yeye anaendelea kusakata kabumbu katika timu ya Yanga SC huku Saidi Ntibazonkiza akiwa hana timu hadi kufikia sasa baada ya kuachana na Wekundu wa Msimbazi Simba SC.