UONGOZI wa Yanga umewaingiza kwenye mtego wapinzani wao KMC kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex kwa kuwaambia kwamba itapata ushindi wa pili kwenye mchezo wao ikiwa watafunguka.
KMC baada ya kucheza mechi nne imeambulia ushindi kwenye mchezo mmoja na ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua kwamba wanaamini KMC ni timu bora na inaweza kuifunga Yanga kwenye mchezo wao ikiwa watafunguka na kucheza bila kuweka walinzi wengi kwenye mchezo huo.
“KMC ni timu nzuri na nina amini kwamba inaweza kutufunga na ikapata ushindi mchezo wake wa pili dhidi ya Yanga ikiwa watafunguka na kucheza mpira kwani tunatambua uimara wake.
“Sio wanakuja kuweka walinzi 9 sijui na mshambuliaji mmoja kisha ikifungwa bao moja inakwenda kufanya sherehe hiyo hapana utakuwa sio mpira ndio maana ninawaambia kwamba waje kucheza mpira hilo lnawezekana na watoe burudani.”
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa tatu usiku kwa timu zote kusaka pointi tatu.