Kikosi cha Mnyama, Simba SC, kiliwasilia Jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa raundi ya nne wa Ligi Kuu Bara.
Katika mechi hii, Simba SC itakabiliana na Dodoma Jiji FC, ambao watakuwa wakicheza mchezo wao wa sita siku ya leo, Jumapili, Septemba 29, 2024, katika dimba la Jamhuri Dodoma.
Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, amethibitisha kuwa atawakosa nyota wake watatu muhimu katika mchezo huo.
Wachezaji wanaokosa ni Joshua Mutale, Mzamiru Yassin, na Yusuph Kagoma, kutokana na sababu mbalimbali za kiafya na majeraha.
Hali hii inawafanya mashabiki wa Simba SC kuwa na wasiwasi kuhusu uwezo wa timu yao kushindana katika mechi hiyo bila wachezaji hawa muhimu.
Fadlu Davis amesisitiza kuwa kikosi chake kimejiandaa vizuri na kwamba wana mategemeo makubwa ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.
Anasema kuwa timu inahitaji kujituma zaidi ili kukabiliana na changamoto zilizopo, hususan dhidi ya Dodoma Jiji FC ambao wana uzoefu katika mchezo wa nyumbani.