Shabiki wa klabu ya Mallorca aliyekutwa na hatia ya kumfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi mshambuliaji wa Real Madrid Vinicius Jr mwaka 2023 amefungwa jela miezi 12 na mamlaka za sheria nchini Hispania.
Shabiki huyo ambaye pia alikutwa na hatia ya kumbagua mchezaji wa Nigeria na Villareal Samuel Chukwueze amefungiwa kuhudhuria viwanja vya michezo kwa miaka mitatu.