KIUNGO wa Yanga Jonas Mkude maarufu kama Nungunungu amefunguka na kusema kwamba, yeye kama mchezaji hajawahi kumroga mchezaji mwenzake Mganda Khaled Aucho.
Mkude aliyesajiliwa na Yanga msimu juzi, amekuwa na nafasi finyu ya kucheza katika klabu hiyo, kwa kiasi kikubwa Khaled Aucho ndiye chaguo la kwanza kwa Miguel Gamondi.
“Sisi ni wachezaji na hata kama wote tunacheza namba moja Uwanjani haina haja ya kuleteana chuki kambini au mazoezini na sijawahi kumchukia mwenzangu Khalid Aucho hata kumroga kisa nipate namba sijawahi kiukweli hata Mungu anafahamu hilo.
“Aucho mimi kwangu ni kama Kaka yangu najifunza mengi kutoka kwake hata tukiwa mazoezini na kama anapata namba mbele yangu Kocha yeye ndio anajua umuhimu wa mchezaji wake kumtumia kwenye mechi Uwanjani kwasababu yeye ndio mkuu wetu” Kiungo wa Yanga SC Jonas Mkude.