Baada ya jana Argentina kuwachapa Chile 3-0 nyumbani, nahodha wa timu hiyo Lionel Messi alimtumia barua ya wazi ya kushukuru kwa utumishi Angel Di Maria ambaye pia shirikisho la soka nchini Argentina liliutumia mchezo huo kuwa sehemu ya kumuaga baada ya kustaafu rasmi kuichezea timu hiyo.
“Natumai wewe, familia yako na wapendwa wake mmefurahia jioni ya leo, tumesema kila kitu tulichopaswa kusema, tulishirikiana vyema kwenye kila jambo hadi ulipofika mwisho kama huu, tunakupenda na tutakukumbuka sana” ilisema sehemu ya barua ya Messi kwa Di Maria.
Di Maria alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo baada ya michuano ya Copa America ambapo Argentina walitwaa Ubingwa.